ALICHOSEMA Msuva kuhusu Tanzania kufuzu fainali za AFCON


Baada ya ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya DR Congo katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotambulika na kalenda ya Fifa, Mshambuliaji wa Taifa Stars  na klabu ya Difaa El Jadida Simon Msuva anaamini Tanzania inaweza kufuzu na kucheza mashindano ya mataifa ya Afrika.
Msuva amesema unapocheza mechi za kirafiki na kushinda kuna kitu wachezaji wanaongeza kwa hiyo kuna uwezekano wa kufuzu fainali za Afrika.
“Naamini maandalizi yatakuwa mazuri kwa sababu tunavyoshinda kuna kitu tunakipata kwa hiyo tunafurahi na tunaomba uzima ili kila anaewakilisha Tanzania awe mzima katika timu, nafasi ya kufuzu ipo kwa uwezo wa Mungu, uhakika upo kwa sababu ndio timu yetu na sisi ndiyo wakufuzu mkituamini tutafanya kazi”-Msuva
kwa habari mbalimbali endelea kufutilia smilemediatz
pia usisahau kudondosha coment yako

Comments