Mrembo Tunda na Skendo ya Kuchoropoa Mimba Nane za Wanaume Tofaut




Akizungumza na Risasi Jumamosi katika mahojiano hayo maalum, Tunda alisema anashangazwa na madai hayo kwa sababu katika hali ya kawaida mtu huwezi kuchoropoa idadi hiyo ya mimba na bado ukaendelea kufanya shughuli zako kama kawaida.
Alisema katika hali ya kawaida, si rahisi kabisa kwani kama kweli angefanya hivyo, lazima angepata madhara na hata afya yake ingezorota.

“Jamani kweli mtu unaweza kuchoropoa mimba nane tena ndani ya kipindi kifupi? Sidhani kama unaweza ukawa binadamu sahihi kabisa na binafsi sijawahi kutoa mimba kama watu wanavyodai,” alisema Tunda.




 TUMBO LAKE NDO LILIVYO
Mrembo huyo aliendelea kusema kuwa watu wanaweza kumsema hivyo kutokana na tumbo lake lilivyo kwani mara nyingi akifanya mazoezi linapungua, akiacha linakuwa kubwa na watu kudhani ana mimba.

“Hili tumbo wanaweza kulishangaa lakini ni kwamba liko hivyo siku zote kama sijafanya mazoezi muda mrefu na pia sijinyimi kwenye kula chakula kabisa, linakuwa kubwa utadhani nina mimba kumbe walaa,” alisema Tunda ambaye ameuza nyago kwenye video ya Wimbo wa Why Me ya Amini Mwinyimkuu na Elias Barnaba.

Tunda aliongeza kuwa, watu wengi wanamtabiria ana ujauzito kitu ambacho sio kweli kwani hajawahi kushika mimba hata ya kusingiziwa.
“Mimi napenda tu watu wafahamu kuwa sijawahi kushika mimba ya mtu yeyote kama wanavyosema 

 Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na kama ana mpango wa kuzaa naye, Tunda alisema kwa sasa hataki kumuongelea kabisa staa huyo.
“Huyo Diamond naomba nisimuongelee kabisa. Sitaki kuhusishwa naye kwa namna yoyote ile,” alisema Tunda.
zote na wala sijawahi kutoa maana tumbo langu ndivyo lilivyo,” alisema Tunda.

Comments