Real Madrid kukutwa na aibu waliyoikataa Barcelona


Msimu huu unaonakeana sio mzuri sana kwa Real Madrid katika michuano ya La Liga, tayari muda sasa Barcelona wameshaonesha kuwaondoa Madrid katika mbio za ubingwa La Liga msimu huu.
Hili sio jambo la kuumiza sana kwa Real Madrid kwani aibu kubwa kwao inakuja, hili ni tukio la “Guard of Honour” ambapo Madrid wanaweza kujipanga huku na huku ili kuwapigia makofi mabingwa Barcelona.
Barcelona wameongeza pengo la alama na wapinzani wao hadi kufikia alama 11 na hii inamaanisha kwamba kama watawasha moto hivi hivi baasi michezo mitatu kabla ya La Liga kuisha watakuwa mabingwa.
Mchezo kati ya Barcelona na Real Madrid (El Classico) utachezwa zikiwa zimebaki mechi mbili kwa msimu wa La Liga kuisha na El Classico itakuja baada ya Barca kutangazwa kuwa mabingwa wa ligi.
Hii inamaanisha kwamba siku ya mchezo wa huo ndio siku kutakuwa na Guard of Honour hivyo Real Madrid itawapasa kufanya tukio hilo kama heshima kwa mabingwa hao wapya wa La Liga.

kwa habari mbalimbali endelea kufutilia smilemediatz
pia usisahau kudondosha coment yako

Comments