Ben Yedder awaliza Manchester United 2-1

Usiku wa Jumanne ya March 13 2018 ni siku ambayo haikuwa nzuri kwa baadhi ya mashabiki wa soka duniani hususani wanaoshabikia Man United, kwani ndio siku ambayo Club ya Sevilla ya Hispania ili hitimisha safari ya Man United ya michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2017/2018.Man


 United wakiwa katika uwanja wao wa Old Traford katika mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya michuano ya UEFA Champions League wamejikuta wakikubali kipigo cha m
agoli 2-1, magoli ya Sevilla yote mawili yalifungwa na Ben Yedder dakika ya 74 na 78.


Ushindi huo sasa Sevilla unampeleka robo fainali kwa jumla ya magoli 2-1, kwani mchezo wa kwanza waliyocheza Hispania ulimalizika kwa sare tasa ya 0-0, Sevilla ameungana na Real Madrid, Liverpool, Roma, Juventus na Man City waliyofuzu tayari robo fainali ya UEFA 

kwa habari mbalimbali endelea kufutilia smilemediatz

Comments